NAMNA YA KUONGEA ILI MTOTO AKUSIKILIZE NA KUSIKILIZA ILI MTOTO AONGEE

NAMNA YA KUONGEA ILI MTOTO AKUSIKILIZE NA KUSIKILIZA ILI MTOTO AONGEE

PASCAL KANG'IRIA

Psychiatrist

Arusha, Tanzania

Medically reviewed by TherapyRoute
‘’Dhana ya malezi ni uwekezaji wa muda mrefu na sio mkopo wa muda mfupi",

Tangu zama za awali mpaka sasa,jamii ya Dunia imekuwa ikipitia maisha ya kila namna yenye uzuri na ubaya wake ndani.Vizazi kadhaa vimepita vya Wanadamu huku vikiridhishana tamaduni mbalimbali ndani yake.Sehemu kubwa ya kufanya kuleta huu utamaduni kuwa makini na wenye tija imekuwa ni kupitia malezi.Kipindi hiki cha malezi ni kuanzia mimba ya motto mpaka kabla ya kubalehe (wa kiume) au kuvunja ungo (wa kike) . Mchakato huu wa malezi ndio umekuwa ukitumika nyakati zote kuleta ustawi katika jamii mbalimbali za wakazi wa sehemu mbalimbali Duniani.Mchakato huu wa malezi ni mpana sana na wenye mlolongo mrefu sana.Kila jamii imekuwa na utaratibu wake wa kufanya na kutekeleza hili swala na hivyo kufanya pia kila familia kuwa na namna yake ya kutekeleza huu mchakato. Hata ndani ya family moja moja bado utaratibu unaweza kuwa tofauti kwa mtoto mmoja ukilinganisha na mtoto mwingine wa familia hiyo hiyo."Kuzaa mtoto hakutoshi kukufanya kuwa mzazi bora na mwenye kuongoza katika maadili,kama kuwa na kinanda hakufanyi mmiliki kuwa mpigaji mzuri" – Levine. Maelezo ya Mtaalamu Levine yanazidi kutoa mwanga kwa swala hili kuwa linahitaji mkakati kabambe kuweza kufikia lengo lililokusudiwa. Mawasiliano yamekuwa ndio njia pekee inayotumika katika malezi. Hapa naweka mkazo hasa katika namna ya kuyafanya hayo mawasiliano maana ndipo shida nyingi zinazoendelea katika Dunia ya leo zinapoanzia.

Therapy should be personal. Therapists listed on TherapyRoute are qualified, independent, and free to answer to you – no scripts, algorithms, or company policies.

Find Your Therapist

‘’Dhana ya malezi ni uwekezaji wa muda mrefu na sio mkopo wa muda mfupi", mtaalamu mmoja wa malezi alitoa hii hoja.Hoja hii ya uwekezaji katika malezi inaonekana kama haieleweki kwa watu wengi hasa wazazi wenye watoto. Mara nyingi huwa tunajua katika biashara tunahitaji kuwepo ili mambo yaende kama jinsi tunavyohitaji kuwa.Uangalizi wa karibu wa biashara yeyote utahitajika ili kupata matokeo kusudiwa.Mahali pengine mtu aliyewekeza inamlazimu kuweka hata kamera ili kuwa na ufuatiliaji wa karibu wa kila kitu kinachoendelea eneo lake la biashara.Huu uangalizi wa karibu unasaidia kufanya maboresho pale kunapohitaji maboresho ili malengo yafikiwe. Utahitaji kujua muitikio wa wateja wako upoje na hata kujua mahitaji yao ni nini hasa ili uweze kuwatimizia. Kama mzazi ambaye ulihitaji kupata mototo bado unahitaji kumsikiliza mtoto huyo hata ujue anahitaji nini au yupo na nini ili usaidie afikie malengo yake ya maisha ambayo hata wewe kama mzazi hujui anatakiwa kuwa nani au ameandaliwa kuwa nani katika haya maisha hapo baadae. Hitaji la kuwepo karibu na kufuatilia ukuaji wa mtoto wakati wa malezi ni muhimu sana hivyo kipindi cha malezi ni kipindi cha kila mmoja kupata muda wa kumsikiliza mwenzake ili maisha yaoneshe maana.

Kwa sehemu kubwa swala zima la malezi huathiri Afya ya akili ya kiumbe tangu kikiwa tumboni mpaka kipindi chote cha ukuaji wake na mwisho kutengeneza aina fulani ya mtu. Afya ya akili ni uwezo wa kujikubali na kukubali wengine,kupokea na kuchukuliana na hisia ,na kukabiliana na matatizpo na changamoto unazokutana nazo maishani. Kimsingi maisha yetu kila siku ni changamoto na yapo na misukosuko mingi sana. Mtoto anatakiwa kutambulishwa katika aina hii ya maisha vizuri ili kutosha kuwa mtu mwenye manufaa katika maisha yake popote atapokuwa amekwenda.Udhaifu utakaojitokeza katika malezi ya kiumbe,hatimaye huleta udhaifu katika utu wake na mwisho kutosha kushindwa kuwa mtu mwenye manufaa katika jamii atakayo kuwa anaishi. Kila mtu huzaliwa akiwa na vipawa kadha wa kadha ndani yake,mazingira sahihi ya malezi yenye umakini hutosha kufanya vipawa kukuwa na kuwa vya manufaa katika kila jamii atakayo kuja kuishi hapo baadae. Maisha kwa ujumla yapo na mawimbi mengi amabyo kwa kiasi kikubwa yasipowekewa namna nzuri ya kuyakabili basi yataharibu mifumo yote makini katika maisha ya mtu na kuharibu Afya yake ya Akili.Namna bora ya kukabiliana na mawimbi ya aina zote ya maisha tunaipata kupitia aina ya malezi mtu atakayoyapitia kipindi chote cha kuaanzia kutungwa kwa mimba yake mpaka wakati wa kubalehe ama kuvunja ungo.Kimsingi MALEZI MAKINI sio jambo rahisi na huenda yasiwe na njia moja ya kufika katika hitimisho tazamiwa. "Wakati mzuri wa kuzuia ulimi wako ni pale ambapo unajisikia kuwa ni lazima uongee kitu" - Josh Billings. Wazazi wengi huwa ni waongeaji na watoa maelezo mara kwa mara wakiamini hii ndio nia sahihi ya kufanya ili mambo yaweze kwenda. Wakati pale unakuwa umechafukwa hasa basi sio muda sahihi wa kuongea kitu."Watoto wangu kamwe hawasikilizi neno lolote kutoka kwangu" alisikika mama mmoja akisema. Mwingine akasema "Mara zote nikimuuliza mtoto wangu swali,anapandisha mabega na kunijibu kwa kifupi,nitafanyaje ili aweze kuongea".Kijana mmoja alisema 'Ninapojaribu kufungua mdomo wangu kuongea,napata ishara ya kukatishwa kuongea na Baba na kama nikiulizwa swali huwa napata jibu la silabi moja tu" Kila mtu anapoongelea elimu ya malezi ,anasisitiza mawasiliano kwa watoto, ukweli ni huu mara zote huwa tunawasiliana ( kwa maneno au vitendo)

Lakini swali la muhimu ni hili,Je?Unawasiliana? Kujua nini na kwa namna gani unawasiliana ni rahisi kuliko kuwasiliana. Kulingana na Oxford English Dictionary,maneno ya Kiingereza ya kawaida kama mia tano yana maana tofauti tofauti zaidi ya 23, hivyo kuna uwezekano mkubwa ya kila unachowasiliana na mwanao kisiwe na maana halisi ya unachokizungumza. Mfano; Maneno ya Wazazi - 'Huwa hunisikilizi ninaposema" // " Kumbuka kuwa mwema" // "Ulikuwa nyumbani kwa Bibi yako.." - Je? Mwanao anakuelewa? Tangu watoto kuwa na uwezo mkubwa wa kufikiri,huwa wanapata shida sana kuelewa kauli ambazo hazipo wazi sawa sawa. Wazazi makini wanatumia ujumbe sawa sawa / uwazi na kuondoa utata katika lugha wanayotumia,mfano wa ile kauli "Kumbuka kuwa mwema" ambapo Mtoto James aliambiwa katika sherehe yake ya siku ya kuzaliwa. Ingepaswa kuwa hivi,Kumbuka kumshukuru Chacha na Mama yake kwa muda wao walioutoa kuja kwenye sherehe yako.

HITIMISHO

Ujumbe sahihi unamfundisha mtoto wako kuwa na tabia iliyo njema. Mfanye mwanao kujua pale anapofanya vizuri na pale anapokosea umsaidie kurekebisha tabia. Hakuna mtoto mwenye tabia mbaya au mtoto mbaya,kila mtoto huja akiwa safi ila huharibiwa hasa na tabia za wazazi wake na hayo mazingira anayokulia ambayo hata hivyo hao Wazazi wake ndio walimuweka katika hayo mazingira. Kama Mzazi kuwa makini sana katika maongezi yako lakini pia kuwa makini sana katika matendo yako/ tabia yako. Watoto wapo hivi tunavyowaona kutokana na aina ya wazazi alionao na jinsi wanavyomtambulisha katika hii Dunia. Zaidi ya yote,Mtoto wako anaposikia ujumbe sahihi ( maneno au matendo ) kutoka kwako ni rahisi kukujibu au kutenda kwa usahihi pia ( reciprocity)

Important: TherapyRoute does not provide medical advice. All content is for informational purposes and cannot replace consulting a healthcare professional. If you face an emergency, please contact a local emergency service. For immediate emotional support, consider contacting a local helpline.

About The Author

Pascal

Pascal Kang'iria

Psychiatrist

Arusha, Tanzania

I am a mental health practitioner devoted to serving my community. Mental Health services in my context are often poor and many people suffer as a consequence. As a Clinical Psychiatrist, I am the right person to help deal with the demand for mental health services here.

Pascal Kang'iria is a qualified Psychiatrist, based in Ngaramtoni, Arusha, Tanzania. With a commitment to mental health, Pascal provides services in , including Advocacy, Consultation, Corporate Workshops, Group Therapy, Psychiatry, Psychiatry, Supervision & Training, Personal Development and Child Psych & Diagnostic Assessment. Pascal has expertise in .